Staff Service Mail |Sitemap
    
automobile reviews business money buy jewellery finance loans home helps insurance types cosmetics today fitness animals insurance companies in market finance news medical product money us technology in finance time roof repairing places where cook recipes business ideas business pay buy insurance car price in compamy marketing company guide cosmetics product diet info healthy live home decoration tech news auto insurance home improvement online business tips personal loans product reviews security types top business list top company list home tricks weight loss help what kind of business should i start business letter format business case template general business business type it security what is a good business to start business meJe unaridhika na huduma zitolewazo na Taasisi mbalimbali za Serikali zilizopo Mkoa wa Pwani?

Naridhika sana
Naridhika
Sina Uhakika
Siridhiki Kabisa
Siridhiki

Current Results

Welcome

Mkoa wa Pwani ulianzishwa rasmi mwaka 1972. Mkoa wa Pwani upo upande wa Mashariki ya Tanzania Bara.Sehemu kubwa ya Mkoa wa Pwani imepakana  na bahari ya Hindi. Mkoa wa Pwani una ukubwa wa eneo la kilomita za mraba 33,539 . Kati ya kilomita hizo 32,407 sawa na asilimia 96.6 ni eneo la nchi kavu, wakati kilomita za mraba 1,132 sawa na asilimia 3.4 ni eneo la maji.Kiujumla Mkoa wa Pwani ni mkubwa kieneo ukilinganisha na baadhi ya Mikoa mingine hapa nchini.Kiutawala, Mkoa una Wilaya sita ambazo ni Bagamoyo, Kibaha, Kisarawe, Mkuranga, Rufiji na Mafia. Pia Mkoa una jumla ya Halmshauri za wilaya 7 na Halmashauri ya mji 1. Kwa kuzitaja ni Halmashauri za Wilaya za Bagamoyo, Chalinze, Kibaha, Kisarawe, Mkuranga, Rufiji, Mafia na Halmashauri ya Mji Kibaha.

Mkoa wa Pwani una makabila mbalimbali ambapo wenyeji wake ni Wazaramo, Wandengereko, Wakwere, Wadoe, Wamatumbi na Wazigua. Wakazi  hawa shughuli zao za kiuchumi zinategemea Kilimo, ufugaji, uvuvi na biashara ndogondogo katika kujipatia kipato.  Mkoa wa Pwani umepakana na Mikoa minne. Sehemu ya kaskazini kuna  Mkoa wa Tanga, sehemu ya Magharibi utakutana na Mkoa wa Morogoro, sehemu ya Kusini kuna Lindi  na upande wa Mashariki utakutana na Mkoa wa Dar es Salaam. Mkoa upo karibu na Jiji la Dar es Salaam ambapo kiuchumi inakuwa nafuu kwa wakulima na wafanya biashara kwa sababu ya soko kuu la mazao ya chakula na biashara ambalo lipo Dar es salaam.

Uchumi wa Mkoa unategemea sana kilimo ambapo asilimia 78 ya wakazi wake wanajishugulisha na kilimo. Kilimo kinachangia asilimia 60 ya pato la Mkoa na asilimia 40 inachangiwa na sekta za Maliasili, Utalii, Uvuvi, Mifugo, biashara na ajira katika ofisi na asasi mbalimbali.