Mhe Abubakar Kunenge Mkuu wa Mkoa wa Pwani Amefanya ziara ya Ukaguzi wa Miradi ya Umeme kuangalia uzalishaji na Upatikanaji wa Nishati ya Umeme kwa Mkoa wa Pwani.
Kunenge ametembelea na kukagua Ujenzi wa kituo kipya cha Chalinze (400/220/132/32 KV) (Substation) ambacho kitapokea umeme kutoka Kwenye Mradi Bwawa la Mwl Nyerere JNHPP na kusambazwa maeneo mbalimbali ya Nchi na Nchi Jirani,
Kunenge Ameeleza mradi huo unajengwa na Mkandarasi TBEA kutoka China kwa Gharama ya Shilingi Bilioni 130 na kwa awamu ya kwanza ya Ujenzi wa Mradi umefikia Asilimia 17 na utakamilika ifikapo Januari 2023.
Ameeleza awamu ya kwanza kituo kitakuwa na Uwezo wa kupooza Megawatt 1000 na Awamu ya pili ni Megawatt 1115, Ameeleza Matarajio yake baada ya kukamilka ni kupata Umeme wa Uhakika kwa Wilaya zote za Mkoa wa Pwani."Kongani zote za Viwanda zitapata Umeme wa Uhakika" Ameeleza Kunenge.
Kunenge amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluh Hassan kwa kuendeleza Ujenzi wa Miundombinu ya Umeme, Maji na Barabara kwa Mkoa wa Pwani.
Ametoa Rai kwa Vijana watakao pata Ajira kwenye Mradi huo kufanya kazi kwa bidii na maarifa na kuepukana na Wizi na kuhakisha kila lilipangwa linakamilika.
katika hatua nyingine Kunenge amekagua Kituo cha Mlandizi ambao kwa sasa kina Uwezo wa MVA 120 Ameeleza Serikali ipo kwenye mpango wa kuongeza Transfoma mbili zenye Uwezo wa MVA 180 na kufikia MVA 300 kwa kituo hicho Ameeleza gharama za maboresho hayo yatagharimu Shilingi Bilioni 20.
Aidha, Kunenge amekagua Ujenzi wa Kituo cha kupooza Umeme cha Luguruni (Luguruni substation) Ameeleza kuwa kituo hicho kina Transfoma mbili za MVA 90 kila mmoja na Mradi huo umegharimu Shilingi Bilioni 15.5, Ujenzi umefikia Asilimia 97 na tayari wamewasha na kunganisha line ikiwemo kwenye maeneo ya Viwanda TAMCO kibaha.
Ameeleza miradi mingine ni inayoendelea ni pamoja Mradi wa Kituo Mkuranga, Mradi kituo Eneo la Viwanda Zegereni (Bilioni 25) na Kituo Eneo la Viwanda Kwala.
Ameeleza kuwa Miradi hii yote itapelekea upatikanaji wa umeme kuwa wa uhakika na kutakuboresha huduma za kijamii na kukuza uchumi wa nchi kupitia wawekezaji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.