Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Pili Mnyema, ameshiriki maadhimisho ya miaka 58 tangu kuanzishwa kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani – Tumbi. Maadhimisho hayo yamefanyika leo, tarehe 11 Oktoba 2025, katika uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mnyema amewapongeza watumishi wa kada ya afya kwa mchango wao mkubwa katika utoaji wa huduma kwa wananchi, huku akiwaasa kuendelea kufanya kazi kwa weledi, uadilifu, na moyo wa kujituma wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku.
Maadhimisho hayo yamepambwa na maandamano ya amani, michezo mbalimbali kupitia bonanza la afya, pamoja na tukio la kuwaaga rasmi watumishi waliostaafu au kumaliza muda wao wa utumishi katika hospitali hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.