• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • TasksMIS |
    • Events Portal |
Coast Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani

Mchatta awaasa watumishi kufanya kazi kwa weledi ili kutimiza Malengo ya Mkoa

Posted on: March 30th, 2023

Katibu Tawala Mkoa Wa Pwani ,Rashid Mchatta amewaasa watumishi wa mkoa huo kufanya kazi kwa weledi ,kufuata miongozo ya utumishi wa umma ili kutimiza malengo ya kimaendeleo na kuinua uchumi wa mkoa.

Aidha amewataka watumishi hao kumpa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha wanafanikisha Malengo hayo.

Hayo ameyasema leo Machi 30 wakati wa makabadhiano ya Ofisi na aliyekuwa katibu Tawala Mkoa Pwani Zuwena Omary ambae amehamishiwa Mkoani Lindi.

Mchatta ameeleza kila mtumishi atimize wajibu wake kazini na kuwa waadilifu ili kumsaidia Mkuu wa Mkoa huo .

"Kila mtu afanye kazi yake kwa uadilifu wa hali ya juu ili tumsaidie mkuu wa Mkoa kufikia Malengo yake, inapaswa kwenda na kasi ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan pasipo kufanya kazi kwa mazoea "

Nae aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa Zuwena Omary amewataka watumishi hao kumpa ushirikiano Mchatta kama walivyokuwa wakimpa yeye na kupelekea kupiga hatua kwenye baadhi ya Malengo ya Mkoa.

"Binafsi nawashukuru sana watumishi wote wa Ofisi hii kwa ushirikiano mlionipa , ushirikiano ule mkauendeleze kwa Katibu Tawala Mchatta"

Akitoa neno la shukran kwa niaba ya watumishi wote Katibu Tawala Msaidizi Elimu Sara Mlaki amempongeza Katibu Tawala Zuwena kwa uhodari wake wa kazi aliounyesha wakati akiwa Mkoani Pwani.

Katibu Tawala Mchatta amehamia Mkoani Pwani March 2023 akitokea Mkoani Rukwa na aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa Pwani Zuwena Omari Jiri amehamia mkoani Lindi.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC Kunenge Ashiriki Kupiga Kura , Awataka Wananchi wa Pwani kuendelea kujitokeza kwa wingi

    October 29, 2025
  • Dumisheni Umoja na Utulivu kuelekea Uchaguzi Mkuu- Kamati ya Amani Pwani

    October 28, 2025
  • Vituo 3,941 vya kupiga kura vyaandaliwa Mkoani Pwani Kuelekea Uchaguzi mkuu

    October 27, 2025
  • RC Kunenge akabidhi Vitendea kazi vya Zaid ya Sh. Bilion 7 kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Pwani

    October 24, 2025
  • Tazama Zote

Video

Coast Region Investment opportunities
Video Nyingine

Kurasa za Haraka

  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Hotuba za Mkuu wa Mkoa
  • Mpango Mkakati wa Mkoa
  • Investment Opportunity Profile
  • Taarifa mbalimbali kuhusu Mkoa
  • Maktaba ya Picha
  • Barua pepe za watumishi

Tovuti Zinazoshahabiana

  • OR-TAMISEMI
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wakala ya serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Visitors Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

    Sanduku la Posta: 30080 Kibaha

    Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500

    Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500

    Barua pepe: barua@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.