Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo leo Machi, 5 2021 ameendesha Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Maji Vijijini , katika Kikao hicho kilichowakutanisha Viongozi wa Mkoa huo wakiwemo Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wahe. Wabunge na Kamati ya Usalama na Wataalamu wa RUWASA Mkoa Ndikilo amesema
“Hadi kufikia Januari 2021 Wastani wa Asilimia 73 ya Wakazi wote waishio Mkoani Pwani wanapata huduma za Maji safi na Salama. “Hali halisi ya Mkoa wetu ya Upatikanaji wa Huduma ya Maji kwa Mijini nia Asilimia 84% na Asilimia 71% kwa Wananchi waishio Vijijini”. Tunapambana kupata asilimia 14 kwa Vijijini na Asilimia 11 kwa Mijini ili kufikia Lengo lililopo kwenye Ilani ya Uchaguzi wa Chama ya Cha Mapinduzi Alisema Ndikilo.
Ndikilo Amesema Wamekutana kama Viongozi wa Mkoa kujadili namna gani watamsaidia Mhe Rais kufikia Malengo na Maono yake ya kushughulikia shida ya Maji Vijijini , Ndikilo alinukuu Hotuba ya Mhe Rais wakati wa Kulifungua Bunge la 12 kuwa “wakati wa Kampeni za Uchaguzi maeneo mengi aliyopita Mhe Rais alikutana na Shida ya Maji hasa vijijini” Hivyo Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi hiki imedhamiria kuweka nguvu kubwa katika kutatua changamoto ya Maji vijijini. “Tumekutana hapa kama viongozi wa Mkoa huu kujadili namna Maono ya Mhe Rais na Malengo ya kuondoa shida ya Maji yanafikiwaje.”
Ndikilo ametaja Miradi 26 mipya na iliyokarabatiwa ya Maji Vijijini yenye Thamani ya Shilingi Bilioni 3.9 iliyotekelezwa kwa kipindi cha Miaka miwili 2019 hadi sasa na kunufaisha wakazi 38,889. Ameeleza pia Miradi mipya na inayokarabatiwa 48 ya Maji Vijijini inaendelea kutekelezwa yenye thamani ya shilingi Bilioni 9.8 ambayo itanufaisha wakazi zaidi ya 99,334.
Ndikilo amesema Kuwa kwa kuwa Serikali ya Awamu imedhamiria kutatua changamoto ya Maji hasa Vijijini tunatarajia kuletwa kwa fedha nyingi za utekelezaji wa Miradi, Ndikilo ametoa Rai kwa Viongozi wote Mkoani humu kuhakikisha kuwa Miradi yote inatekelezwa kwa ubora, Miradi inaakisi thamani ya Fedha , Miradi ikamilike kwa Wakati na kuhakikisha watumiaji wote wanatunza vyanzo vya Maji na Miundombinu ya Miradi hiyo ili miradi hiyo iwe endelevu. Ametaka pia Taasisi zote za Serikali kuendelea Kulipa Ankara za Maji wanazodaiwa kwa kuwa maji siyo Bure “ Maji ni Bidhaa inayonunulia, (Water is a Commodity and has a Value). Ndikilo ametoa Rai kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya Mkoani humo kutenga maeneo kwa ajili ujenzi wa Ofisi za RUWASA ambayo ni Taasisi Mpya.
Ndikilo ametaka Kupitia kikao hicho kuazimia kuwa kuwa Vyanzo vya Maji vya DAWASA vitumike kupeleka maji maeneo ya Vijijini isisubiri mpaka RUWASA ichimbe visima au mabwawa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.