Mkuu wa Mka wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge leo Agosti 18, 2022 amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa kampuni ya ASTRA Energy INC ya Marekani inayojishughulisha na uzalishaji wa nishati shadidifu na mbolea ambao wameonesha nia ya kuwekeza Mkoani humo.
Katika mazungumzo hayo, Mhe. Kunenge amewahakikishia wawekezaji hao kuwa Serikali ipo tayari kutoa ushirikiano unaohitajika ili kuwezesha makampuni, taasisi na watu binafsi wanaohitaji kuwekeza kutopata vikwazo.
Amesema Mkoa wa Pwani unazo fursa nyingi za uwekezaji katika sekta mbalimbali ambazo zinahitaji wawekezaji kuzichangamkia na akailekeza kampuni hiyo ya ASTRA Energy Inc kukamilisha taratibu zote zinazohitajika ili waweze kuwekeza na kutoa huduma ya nishati kwa wananchi na kufanikisha upatikanaji wa mbolea kwa wakulima ili waweze kuzalisha mazao kwa tija.
"Mazingira ya uwekezaji katika mkoa huu ni mazuri, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan aliahidi na anatekeleza upatikanaji wa miundombinu ya barabara, maji na nishati ya umeme ambavyo kwa pamoja vinachochea uwekezaji na ukuwaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na wa taifa" alifafanua RC Kunenge.
Makamu Rais, uzalishaji nishati ya umeme wa Kampuni hiyo Bw. Tony Thompson alieleza kuwa mpango wao ni kuzalisha nishati shadidifu, mbolea na viua dudu kwa kutumia nguvu ya jua na taka zinazozalishwa majumbani kama malighafi.
"Uzalishaji wetu unalenga kulinda mazingira, tutazalisha umeme kwa mfumo wa unajulikana kama "BOT- Build, Operate and Transfer," alisema Thomson.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.