• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • TasksMIS |
    • Events Portal |
Coast Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani

RC Kunenge awataka Viongozi Kushirikiana

Posted on: September 5th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mheshimiwa Abubakari Kunenge, amehimiza ushirikiano miongoni mwa viongozi wa mkoa huo ili kurahisisha utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Kunenge alitoa kauli hiyo leo, Septemba 4, 2024, wakati wa hafla fupi ya kumwapisha Mkuu mpya wa Wilaya ya Rufiji, Luteni Kanali Fredrick Faustin Komba, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

Alisema ushirikiano ni nguzo muhimu katika kufanikisha mawazo bora kwa ajili ya kutatua changamoto za wananchi na kupanga mipango ya maendeleo kwa kuzingatia uwezo na taaluma za watumishi mbalimbali.

"Huwezi kufanikiwa kama kila kitu unataka kionekane ni kazi yako pekee," alisema Mheshimiwa Kunenge.

Aidha, aliongeza kuwa changamoto za wananchi ni za aina mbalimbali, ambazo zinahitaji wataalamu tofauti kwa ajili ya kuzitatua. Alisisitiza kuwa ushirikiano utawezesha mipango bora ya maendeleo na kutatua changamoto hizo kwa ufanisi zaidi.

Kunenge aliwakumbusha viongozi wa mkoa kufanya kazi kwa mujibu wa mamlaka na majukumu waliyopewa, na kuhakikisha maamuzi wanayofanya ni sahihi ili kuleta maendeleo kwa wananchi. "Hata mtu akikuuliza majukumu yako ni yapi, uwe na uwezo wa kuyaelezea kwa ufasaha," alisisitiza Kunenge.

Vilevile, aliwataka viongozi hao kusimamia ipasavyo ulinzi na usalama pamoja na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambayo ni msingi wa maendeleo kwa wananchi.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Wakuu wa Wilaya wa Mkoa wa Pwani, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mheshimiwa Simon Nickson, aliwahimiza viongozi kufanya kazi kwa weledi ili kuleta matokeo chanya ya maendeleo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Luteni Kanali Fredrick Faustin Komba, aliahidi kutekeleza majukumu yake mapya kwa kufuata sheria na kushirikiana na viongozi wenzake ili kuhakikisha utekelezaji wa sera za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC Kunenge Ashiriki Kupiga Kura , Awataka Wananchi wa Pwani kuendelea kujitokeza kwa wingi

    October 29, 2025
  • Dumisheni Umoja na Utulivu kuelekea Uchaguzi Mkuu- Kamati ya Amani Pwani

    October 28, 2025
  • Vituo 3,941 vya kupiga kura vyaandaliwa Mkoani Pwani Kuelekea Uchaguzi mkuu

    October 27, 2025
  • RC Kunenge akabidhi Vitendea kazi vya Zaid ya Sh. Bilion 7 kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Pwani

    October 24, 2025
  • Tazama Zote

Video

Coast Region Investment opportunities
Video Nyingine

Kurasa za Haraka

  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Hotuba za Mkuu wa Mkoa
  • Mpango Mkakati wa Mkoa
  • Investment Opportunity Profile
  • Taarifa mbalimbali kuhusu Mkoa
  • Maktaba ya Picha
  • Barua pepe za watumishi

Tovuti Zinazoshahabiana

  • OR-TAMISEMI
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wakala ya serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Visitors Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

    Sanduku la Posta: 30080 Kibaha

    Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500

    Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500

    Barua pepe: barua@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.

  • Situs Toto
  • Situs Slot Gacor
  • AXL777
  • Situs Toto
  • AERO88
  • Situs Slot Gacor
  • DORA77
  • DORA77
  • DORA77
  • Toto Togel
  • Situs Toto
  • AXL777
  • AERO88
  • Situs Slot Gacor
  • Situs Slot Gacor
  • Situs Toto
  • Toto Slot Gacor
  • Toto Slot
  • Toto Slot
  • DORA77
  • KOI200
  • KOI200
  • SILVAWIN
  • AXL777
  • YAMITOTO
  • NABITOTO
  • YAMITOTO
  • KOI200
  • KOI200
  • KOI200