Pwani umefanikiwa kuhoji zaidi ya asilimia 40 ya Kaya katika Sensa (ukusanyaji taarifa za watu na makazi) hadi kufikia jioni ya Agosti 23, 2022.
Akitoa taarifa Kwenye kikao cha tathmini juu ya mwenendo wa Sensa kilichoitishwa na kuongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge alisema kuwa zoezi hilo linaendelea vizuri mkoani kwake na kuwa changamoto ndogondogo zilizojitokeza zilitatuliwa na shughuli hiyo inaendelea vizuri.
Katika kikao hicho kilicho, Mhe. Majaliwa aliwapongeza Wahe. Wakuu wa Mikoa, wa Wilaya pamoja na kamati zao za Sensa kote nchini kwa jitihada kubwa wanazozifanya kuhamasisha na kuelimisha umma kujitokeza kuhesabiwa na kutoa taarifa sahihi pamoja na kuwaandaa makarani na kamba matokeo ya hali hiyo yameonekana kwa kuwa zoezi limeanza na linaendelea vizuri.
Mhe. Majaliwa pia ameelekeza kuimarishwa mawasiliano kati ya mikoa, wilaya na ofisi za takwimu na ikiwa ni pamoja na kuendelea kuhamasisha umma ili watu wote wafikiwe na kuandikishwa.
Aidha, Waziri Mkuu ameonya dhidi ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii kupotosha taarifa za Sensa na akaelekeza wadhibitiwe kwani zoezi hilo ni la heshima.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.