• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • TasksMIS |
    • Events Portal |
Coast Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani

RC Ndikilo apokea masaada wa mifuko ya Saruji 300 kutoka Kisarawe cement

Posted on: October 9th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo,amepokea msaada wa mifuko 300 ya saruji yenye thamani ya Sh milioni nne kutoka katika kampuni ya uzalishaji wa saruji ya Kisarawe Cement iliyopo katika Wilaya ya Kisarawe Mkoani humu.

Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika mwanzoni mwa wiki hii  jana katika viwanja vya Ofisi ya  Mkuu wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo huku likishuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo katibu tawala wa Mkoa bibi  Theresia Mmbando na wataalam wengine kutoka sekretarieti yaMkoa Pwani.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo mkurugenzi mkazi wa kampuni hiyo Samir Jaffar,alisema kuwa lengo la kutoa msaada huo ni kuunga mkono  jitihada za Mkuu wa Mkoa katika kukarabati kiwanja cha kufanyia maonyesho ya bidhaa za viwandani yanayotarajiwa kufanyika mwisho mwa Oktoba mwaka huu.

Jaffar,alisema kuwa katika awamu ya kwanza wameamua kuchangia mifuko 300 ya saruji yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni nne na kwamba msaada huo utaendelea kutolewa kadri ya mahitaji huku akiomba ushirikiano na Serikali katika kuhakikisha bidhaa zao zinapata masoko ya uhakika.

"kampuni yetu inatambua mchango wa mkuu wa Mkoa katika jitihada za kuinua sekta ya viwanda mkoani kwetu lakini na sisi tupo tayari kuungana na mkuu huyu pamoja na Rais Dkt.John Magufuli kwa harakati ya kuwa na Tanzania ya viwanda hivyo tutaendelea kuchangia katika masuala yote ya maendeleo,"alisema Jaffar

Aidha,Jaffar alisema kuwa kwasasa kiwanda chao kinazalisha tani 300 na hii inatokana na kuwepo kwa miundombinu ya barabara ya kusafirisha bidhaa hiyo kuwa mibovu kwani kwasasa barabara wanayolazimika kuitumia kutoka Kisarawe kupitia Kiluvya inatakiwa gari libebe chini ya tani 10 jambo ambalo linakwamisha uzalishaji.

Alisema ,kwasasa uwezo wao ni kuzalisha tani 500 lakini hatahivyo wanashindwa kutokana na changamoto hiyo lakini kama miundombinu itakuwa sawa ni wazi kuwa wataweza kuzalisha zaidi na kwamba malengo yake makubwa ni kuhakikisha kiwanda hicho kinazalisha tani elfu kumi na kuendelea ambapo aliomba Serikali kunagalia namna ya kutatua changamoto hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo,aliishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo huku akisema saruji hiyo itatumika katika kukarabati uwanja wa maonyesho ya bidhaa za viwandani uliopo Picha ya Ndege Kibaha ambapo kukamilika kwa uwanja huo utasaidia kufanyika kwa maonyesho hayo yanayotarajia kuanza Oktoba 29 mwaka huu.

“Mkoa wa Pwani umekuja na mikakati ya kufanya maonyesho hayo kila mwaka ambapo kwa mwaka huu mkoa unamahitaji makubwa katika kukarabati uwanja huo na kwamba anaimani baada ya kukamilika kwa uwanja huo wazalishaji wa bidhaa za viwandani watapata fursa ya kutangaza bidhaa zao kupitia maonyesho hayo” alisema Mhandisi Ndikilo.

Akizungumzia changamoto za barabara zilizotolewa na wamiliki wa kiwanda Kisarawe Cement,alisema kuwa Mkoa unajipanga kukabiliana na changamoto hiyo ili kuweza kutoa fursa kwa wawekezaji hao kupata unafuu wa kusafirisha bidhaa zao na hivyo kupanua wigo wa kiuchumi kwa wananchi na hata wawekezaji hao.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC Kunenge Ashiriki Kupiga Kura , Awataka Wananchi wa Pwani kuendelea kujitokeza kwa wingi

    October 29, 2025
  • Dumisheni Umoja na Utulivu kuelekea Uchaguzi Mkuu- Kamati ya Amani Pwani

    October 28, 2025
  • Vituo 3,941 vya kupiga kura vyaandaliwa Mkoani Pwani Kuelekea Uchaguzi mkuu

    October 27, 2025
  • RC Kunenge akabidhi Vitendea kazi vya Zaid ya Sh. Bilion 7 kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Pwani

    October 24, 2025
  • Tazama Zote

Video

Coast Region Investment opportunities
Video Nyingine

Kurasa za Haraka

  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Hotuba za Mkuu wa Mkoa
  • Mpango Mkakati wa Mkoa
  • Investment Opportunity Profile
  • Taarifa mbalimbali kuhusu Mkoa
  • Maktaba ya Picha
  • Barua pepe za watumishi

Tovuti Zinazoshahabiana

  • OR-TAMISEMI
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wakala ya serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Visitors Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

    Sanduku la Posta: 30080 Kibaha

    Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500

    Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500

    Barua pepe: barua@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.

  • Situs Toto
  • Situs Slot Gacor
  • AXL777
  • Situs Toto
  • AERO88
  • Situs Slot Gacor
  • DORA77
  • DORA77
  • DORA77
  • Toto Togel
  • Situs Toto
  • AXL777
  • AERO88
  • Situs Slot Gacor
  • Situs Slot Gacor
  • Situs Toto
  • Toto Slot Gacor
  • Toto Slot
  • Toto Slot
  • DORA77
  • KOI200
  • KOI200
  • SILVAWIN
  • AXL777
  • YAMITOTO
  • NABITOTO
  • YAMITOTO
  • KOI200
  • KOI200
  • KOI200