Waganga Wakuu wa Wilaya Mkoa wa Pwani watakiwa kuhakisha Zahanati na Vituo vyote vya Afya vinakuwa wazi masaa yote, siku Saba katika juma hasa Vijijini penye wananchi Wengi ili kuhudumia Wanachi.
Rai hiyo ameitoa Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa Kikao cha tatu cha nusu mwaka Julai- Desemba 2020 Cha Tathmini ya Mktaba wa Lishe na CHF iliyoboreshwa Mkoa wa Pwani leo Aprili 14, 2021 katika Ukumbi wa Mikutano uliopo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa-Kibaha
Akizungumza kwenye kikao hicho Ndikilo amesisitiza kuwa "Nchi yetu haijapungukiwa wataalamu, mambo kama haya ya Wataalamu kufunga vituo vya Afya na Zahanati si ya kufumbia macho hata kidogo, ikibainika kituo kimefungwa wahusika wachukuliwe hatua ikiwepo kuachishwa kazi" alisema Ndikilo
Amewataka Viongozi wa Mkoa huo kuwa na utaratibu wa kutembelea Zahanati na Vituo vya Afya na kuchukua hatua pale wanapokuta vituo hivyo vimefungwa, na husababisha wananchi kukosa huduma.
Ndikilo ameeleza Wananchi kufika na kukosa huduma katika Vituo vya Afya na Zahanati kunasababiasha kushusha ari ya Wananchi kujiunga na CHF iliyoboreshwa katika Mkoa huo.
Amewataka Viongozi wa Dini kuhimiza Waumini wao kujiunga na CHF iliyoboreshwa katika Nyumba zao za ibada
Ameeleeza hali ya usajili katika mfuko wa Bima ya afya ya jamii (CHF) iliyoboreshwa hairidhishi ,hadi Machi,2021 ni kaya 10,038 pekee sawa na asilimia 5.1 zimejiunga na mfuko huo kati ya kaya 294,634.
Kuhusu Lishe Ndikilo Ameeleza kwa Mwaka uliopita Mkoa huo ulishika nafasi yaTano Bora katika Mikoa yote, Ameeleza kuwa Lishe Bora Ni kichocheo cha maendeleo endelevu, ametaja hali ya udumavu Mkoa huo ni Asilimia 23.8% ukilinganisha na taifa wa Asilimia 30.1,
Ndikilo amesema Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa Mkoa hauridhishi hususani katika kiashiria Cha utoaji wa Fedha kwa ajili ya Utekelezaji wa Shughuli za Lishe. Amewataka Wakurugenzi kutoa Fedha ili Utekelezaji wa Lishe ufanyike.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.