Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Shangwe Twamala amesisitiza ulazima wa Taasisi za Umma kutumia mfumo wa kielektroniki wa ununuzi wa Umma “NeST” ambao unasimamiwa na mamlaka ya udhibiti wa ununuzi wa Umma(PPRA).
Hayo ameyasema Juni 24,2024 wakati akifungua mafunzo ya siku tano juu ya Mfumo wa NeST kanda ya Pwani yaliyofanyaki Wilayani Bagamoyo.
Twamala ameeleza kwamba matumizi ya mfumo huu ni maagizo ya Serikali hivyo mahitaji yote katika ofisi za Umma lazima yanunulliwe kwa kutumia mfumo huo.
Ameeleza zaidi kuwa Waraka namba 2. wa Hazina unaotaka taasisi zote za Umma kufanya manunuzi kupitia mfumo wa NeST
Pamoja na kuwa matumizi ya mfumo ni agizo la Serikali pia ni matakwa ya sheria yanayobainishwa katika sheria mpya ya ununuzi sheria no 10 ya mwaka 2023
Ameeleza kuwa mfumo huo ni rahisi na rafiki kuutumia . Pia umesaidia kuondoa tabia za urasimu iliyokuwa ikijitokeza kipindi cha mfumo wa Zamani pia umeongeza ushirikishawaji wa watumiaji kwa kuwa wanaomba mahitaji kwa kutumia mfumo.
"Mfumo huu wa NeST umeleta uwazi zaidi ukilinganishwa na ule wa awali wa TANePS ambao ulikuwa na changamoto mbalimbali ambapo ushirikishwaji ulikuwa mdogo sana na uliruhusu baadhi ya taratibu za ununuzi kufanyika nje ya Mfumo.
Katika hatua nyingine Twamala aliishauri PPRA kuweka mikakati ya kuhakikisha wanapata washiriki wengi katika mafunzo ili mfumo huu ufahamike na watumiaji wengi .
Twamala aliipongeza PPRA kwa kuendelea kuwa wabunifu kwa kutumia wataalamu mbalimbli wa TEHAMA na sheria kuhakikisha ununuzi wa mahitaji ya Umma unafanyika kwa uwazi ili kuongeza tija katika kupata mahitaji kwa haraka na yenye thamani halisi ya fedha
Mafunzo hayo yamewashirikisha watumiaji wa mfumo kutoka taasisi mbalimbali za Umma kutoka mkoani Tanga, Morogoro na Pwani.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.